Serikali ya Misri, imekanusha madai kuwa imeamua kufutilia mbali vuguvugu la Muslim Brotherhood.
Msemaji katika wizara ya maswala ya kijamii,
alinukuliwa akisema kuwa wizara itafutilia mbali hadhi ya vuguvugu hilo
kama shirika lisilo la kiserikali katika siku chache zijazo.
Lakini taarifa kutoka katika ofisi
ya waziri mkuu Sherif Shawki, alisema kuwa waziri wa maswala ya kijamii
bado hajatoa taarifa rasmi kuhusu uamuzi wake.
Maafisa wa kijeshi, wameanzisha msako mkubwa
dhidi ya vuguvugu hilo tangu kuondolewa mamlakani kwa aliyekuwa rais na
kiongozi wa chama hicho, Mohammed Morsi.
Mamia ya maafisa wakuu akiwemo Generali Mohammed Badie,wamezuiliwa kwa madai ya kuchochea ghasia na mauaji.
Mamia ya watu wanaotaka Morsi aachiliwe pia
wameuawa kwenye makabiliano na maafisa wa usalama wanaosema kuwa
harakati zao ni vitendo vya ugaidi.
Vuguvugu hili lenye miaka 85 liliharamishwa
Misri mwaka 1954, ingawa likajisajili kama shirika lisilo la
kiserikali,mnamo mwezi Machi.
Muslim Brotherhood pia lina tawi lake la kisiasa
lililosajiliwa kama-chama cha Freedom and Justice kilichoundwa mwaka
2011 mwezi Juni baada ya mapinduzi ya Hosni Mubarak.
CHANZO : BBCSWAHILI
No comments:
Post a Comment