Kaimu Mkuu wa Idara ya Huduma za Kibenki kwa Kufuata Kanuni za Kiislamu
(Islamic Banking), wa Benki ya NBC Tanzania, Yassir Masoud (katikati)
akizungumza katika droo ya awamu ya pili kupata washindi wawili
waliojishindia safari wao na wenza wao inayolipiwa kila kitu na NBC
kushiriki ibada ya Hija mjini Makka nchini Saudi Arabia baadae Mwezi
ujao. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wengine kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa NBC, Alina Maria Kimaryo,
Meneja Uhusiano wa benki hiyo, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi wa Bodi
ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
Meneja
Uhusiano wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Eddie Mhina akipiga simu
kwa mmoja wa washindi wa kampeni ya Islamic Banking ya benki hiyo ambayo
washindi wawili na wenzao wao watalipiwa gharama zote kwenda Makka
nchini Saudi Arabia kushiriki ibada ya Hijja baadae mwezi ujao. Wengine
kutoka kushoto ni Meneja Masoko wa benki hiyo, Alina Maria Kimaryo,
Kaimu Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud na Mkaguzi
Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi
Abdulhussein.
Mkaguzi
Mwandamizi wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi
Abdulhussein (katikati) akihakiki majina ya washindi wa kampeni hiyo.
Wengine kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa Huduma za Kibenki kwa kufuata
kanuni za Kiislamu wa NBC, Yassir Masoud na Meneja Uhusiano wa benki
hiyo, Eddie Mhina pamoja na baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria
hafla hiyo.
Kaimu
Mkuu wa Islamic Banking ya NBC, Yassir Masoud (katikati) akifurahi
pamoja na baadhi ya maofisa wa benki hiyo wakati baadhi ya washindi
wakielezea furaha yao baada ya kupigiwa simu na kujulishwa kujishindia
safari ya kwenda hijja itakayolipiwa kila kitu na NBC. Kutoka kushoto ni
Ofisa katika Idara ya Operesheni, Edesia Kahyarara, Meneja Masoko,
Alina Maria Kimaryo, Meneja Uhusiano, Eddie Mhina na Mkaguzi Mwandamizi
wa Bodi ya Michezo ya Kubahatisha Tanzania, Humudi Abdulhussein.
No comments:
Post a Comment