Tuesday, September 03, 2013

WANANCHI WA MOROGORO VIJIJINI WASHIRIKIANA NA MBUNGE WAO KATIKA SHUGHULI ZA MAENDELEO

Mbunge wa Jimbo la Morogoro kusini Mh Innocent Kalogeris akiwa katika shuguli za maendeleo jimboni .Mbunge huyo alishirikiana na wanachi wa Kijiji cha kiswila kufyatua matofali kwa ajili ya ujenzi wa madarasa, Zahanati na Nyumba za walimu.Kijiji hiko wamejiwekea Lengo la Kufyatua matofali Laki moja.Kijiji hiko kinaundwa na vitongoji vya Mng’ombe ,Kiswila Lumula Na Gubi.
Mbunge huyo akionyesha mfano wa kufyatua matofali ambapo jumla ya matofali 5000 yalifyatuliwa .Mbunge huyo pekee alifyatua matofali 600.Ambapo Mpaka sasa tofali Elfu 20000 zimeshafyatuliwa tayari kwa ajili ya Ujenzi utakaoanza mara moja.
Mbunge Inno Kazini.Walinichagua nishirikiane nao na si kuwakimbia.Maendeleo ya jimbo letu yataletwa na sisi wananchi wa jimbo hili
Wananchi wa kijiji hicho wakishirikiana na Mbunge wao katika Shuguli hiyo jana
 

Wakina mama Wa kijiji hicho waliojitokeza katika Shuguli hiyo kwa ajili ya maendeleo ya kijiji chao
Mbunge huyo akiaongea na wananch wa kijiji hico mara baada ya kuwahamasisha kufanya shuguli za kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Jimbo la Morogoro Kusini

No comments:

Post a Comment