Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman Kova akitoa hotuba yake wakati akizindua mradi wa
ulinzi ngazi na familia mkoa wa Kinondoni Tarafa ya Kinondoni leo
Octoba 11-2013 kwenye viwanja biafla jijini Dar es salaam,pia amewataka
wananchi kutoa taarifa kwenye jeshi la polisi watu ambao wanaishi nao
wasikubali kukaa na watu ambao hawajui kazi wanazofanya.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni, Camillus Wambura akielezea mikakati wanaopambana na wahalifu pamoja na kushirikiana na Polisi jamii.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman
Kova akimpa mkono wa pongezi Katibu wa Kampuni ya Suppot Group Bw,Coles
Scott baada ya kuchangia pikipiki 4 aina ya Honda kwaajili ya matumizi
ya Polisi jamii.
Kikosi cha ulinzi shirikishi Polisi jamii wakipita kwa mwendo wa pole mbele ya mgeni rasmi wakati wa uzinduzi wa mradi wa ulinzi ngazi na familia mkoa wa Kinondoni Tarafa ya Kinondoni leo Oktoba 11-2013 kwenye viwanja biafla jijini Dar es salaam.
Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam Suleiman
Kova (watatu kutoka kushoto) akiwa kwenye picha ya pamoja na
wakurugenzi wa makampuni ya ulinzi pamoja na maofisa wa polisi.
PICHA NA PHILEMON SOLOMON WA FULLSHANGWE DAR ES SALAAM
No comments:
Post a Comment