Wednesday, September 04, 2013

KINANA AKUTANA NA BALOZI WA SUDAN


1  
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kulia) akimkaribisha Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali,kabla ya mazungumzo naye, Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Lumumba jijini Dar es Salaam.(Picha na Bashir Nkoromo).
2 

Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (kushoto) akizungumza na Balozi wa Sudan hapa nchini, Dk. Yassir Mohamed Ali, katika Ofisi Ndogo ya Makao Makuu ya CCM, Mtaa wa Lumumba jijini Dar es Saloaam.(Picha na Bashir Nkoromo).

WAZEE YANGA SC WAMKATAA MKENYA NA MUHASIBU MUHINDI…SASA MANJI ANALO JANGWANI

Katika Mkutano wao na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, makutano ya mitaa ya Twiga na Jangwani, Dar es Salaam, Wazee hao wanapinga mambo mawili yaliyofanywa na uongozi wa Manji; kuleta Mhasibu mwenye asili ya Kiasia na kuajiri Katibu mpya kutoka Kenya.
Katibu Mkuu mpya wa Yanga SC, Patrick Naggi yupo tayari nchini kuanza kazi akirithi mikoba ya Lawrence Mwalusako aliyemaliza Mkataba wake.
AKILIMALI MUHIKA NA CHAKUPEWA 

Hatumtaki huyo Mkenya; Kutoka kulia Mzee Bilal Chakupewa, Ibrahim Akilimali na Hashim Muhika. Wazee hao wamesema hawatambui ajira ya Mkenya



Na Zaituni Kibwana,
WAZEE wa Yanga waliokasirika na ‘kuipiga laana’ timu baada ya kutofautiana na aliyekuwa Mwenyekiti wa klabu wakati huo, Wakili Lloyd Baharagu Nchunga ikapigwa 5-0 na Simba SC mwaka juzi, wameingia katika mgogoro mwingine na uongozi wa sasa chini ya Mwenyekiti, Alhaj Yussuf Mehboob Manji. 
Na wazee hao chini ya kinara wao, Ibrahim Ally Akilimali wanaingia katika mtafaruku na uongozi wa Manji, kiasi cha mwezi mmoja na ushei kabla ya mchezo mwingine dhidi ya watani wa jadi, Simba SC Oktoba 20, mwaka huu, Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Akizungumza na Waandishi wa jhabari klabu leo, Mwenyekiti wa Wazee hao, Ibrahim Akilimali amesema kiongozi yeyote ambaye anapaswa kuiongoza Yanga, lazima awe mwanachama wa klabu hiyo, hivyo walivyofanya uongozi ni kinyume kabisa na Katiba inavyotaka.
“Mpaka sasa sisi hatumtambui, kwani hatuna vielelezo vyake vya kuwa mwanachama wa klabu hii, endapo atatuletea vielelezo hivyo sisi tutamtambua na kumpa ushirikiano.
“Kazi za Wanayanga zitafanywa na wanachama wetu pekee na si wa nje ya klabu yetu, hatutakubali hata chembe kuona katiba yetu ikikanyagwa na viongozi wetu, tutasimama kidete mpaka mwisho kuona jambo hili halifanikiwi,” alisema Akilimali
Alisema wao wakiwa kama wanachama wa Yanga hawatambui ajira ya raia huyo wa Kenya na anatakiwa kuondoka ndani ya saa 24 klabuni hapo.
Akilimali alisema hawataki kumwona katika klabu hiyo, kwani Yanga ina wasomi wengi ambao wanaweza kuifanya kazi hiyo.
Alimfananisha Mkenya huyo ni mtu aliyeingia kwa njia za panya katika klabu hiyo, kwa kuwa hawana mwanachama wa aina yake kwenye leja ya wanachama wa Yanga.
Alisema wamekuwa na kawaida ya kupewa taarifa na Mwenyekiti wa Klabu hiyo, Manji kama kunakuwa na jambo lolote ambalo wamepanga kulifanya kwa maslahi ya Yanga, lakini hawakuambiwa kuhusu ajira ya Mkenya huyo.
“Huyu mtu tunamwona ni ‘kanjanja’ aondoke haraka sana, sisi wana Yanga hatumuitaji kabisa,” alisema Akilimali.
Wakati huo huo, mwanachama wa klabu hiyo, Said Motisha alisema Yanga itagawanyika kwa hilo, kwani hawatakubali wazawa kunyimwa ajira wakati wanasifa ya kufanya kazi.
CHANZO CHA HABARI HII: BLOG YA BIN ZUBEIRY LEO MCHANA

MKUTANO WA SADCOPAC WAENDELEA ARUSHA

Mkutano wa 10 wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka Mabunge ya Nchi  wananchama wa SADC ujulikanao kama (SADCOPAC) unaendelea jijini Arusha, ambapo kamati ya Bunge ya PAC ndio mwenyeji wa Mkutano huo.
A  

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akiwasilisha Taarifa ya Tanzania ya utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 8 na 9 ikiwa ni matakwa ya Wajumbe wa Mkutano huo ambapo kila Nchi wanachama huwasilisha taarifa hiyo.
B  

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akiwasilisha Taarifa ya Tanzania ya utekelezaji wa Maazimio ya Mkutano wa 8 na 9 ikiwa ni matakwa ya Wajumbe wa Mkutano huo ambapo kila Nchi wanachama huwasilisha taarifa hiyo.
C 

 Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akimweleza jambo Mwenyekiti wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) ambaye pia ni mwenyekiti wa PAC kutoka Bunge la Afrika Kusini Mhe. Sipho Makama wakati wa mapumziko ya Mkutano wa 10 wa SADCOPAC unaendelea Arusha.
D  

Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (PAC) Mhe. Zitto Kabwe akiuliza swali wakati wa majadiliano ya mkutano wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) unaoendelea Arusha.
F 

Mjumbe wa Mkutano wa Mwaka wa SADCOPAC kutoka Tanzania Mhe. Asumpta Mshama akiuliza swali wakati wa majadiliano ya mkutano wa Umoja wa Kamati za Bunge za Hesabu za Serikali kutoka nchi zilizo kusini mwa jangwa la sahara (SADCOPAC) unaoendelea Arusha. Tanzania imewasilisha utekelezaji wa maazimio ya mikutano ya 8 na 9 katika mkutano huo. 
Picha na Bunge

MATUKIO KATIKA TASWIRA BUNGENI MJINI DODOMA LEO

IMG_1322  

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na Naibu Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, Ummy Mwalimu  kwenye viawnja vya Bunge Mjini Dodoma  Septemba 4, 2013. (Picha na ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_1326  

Naibu Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Adam Malima   kwenye Ofisi za Bunge Mjini Dodoma Septemba 4, 2013. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
IMG_1338 

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizungumza na wabunge wa Viti Maalum, Fatuma  Mikidadi (kulia)  na Rukia Kassim Ahmed. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AMUAPISHA WAZIRI WA FEDHA

IMG_3934  

Waziri wa Uwezeshaji,Ustawi wa Jamii,Maendeleo ya Vijana Wanawake na Watoto Zainab Omar Mohamed,(kushoto) Waziri Machano Omar Saidi,na Waziri Haji Faki Shaali,(hawana Wizara maalum) na Waziri wa Miundombinu na Mawasiliano Rashid Seif,(kulia) wakiwa katika ukumbi wa mikutano Ikulu Mjini Zanzibar kushuhudia kuapishwa kwa Omar Yussuf Mzee kuwa Waziri wa Fedha, leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3945  

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akimuapisha Omar Yussuf Mzee,kuwa Waziri wa Fedha,katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]
IMG_3953 

Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akiwa katika picha  Omar Yussuf Mzee,baada ya kumuapisha kuwa Waziri wa Fedha,katika hafla iliyofanyika Ukumbi wa Ikulu Mjini Zanzibar leo asubuhi.[Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.]

MWENGE WA UHURU WAKABIDHIWA RASMI MKOA WA DAR ES SALAAM


Picture 394
Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa Juma Ali Simai akitoa salamu za shukrani kwa Mkuu wa Mkoa wa Pwani Hajati Mwantum Mahiza (aliyevaa Miwani) kabla ya kuukabithi Mwenge huo kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.

Picture 324  

Mkuu wa Wilaya ya Mafia Sauda Salum Mtondoo(kulia) akimkabidhi Mwenge wa Uhuru Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) kwa ajili ya kuukabidhi Mwenge kwa Mkoa wa Dar es Salaam, katika makabidhiano yaliyofanyika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.


Picture 396 

Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Michezo Kutoka Wizara ya Habari,Vijana,Utamaduni na Michezo Leonard Thadeo(kushoto) akipokea Mwenge wa uhuru kutoka kwa Mmoja wa wakimbiza mwenge kitaifa, katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture 398 

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki (kulia) akikabidhiwa Mwenge wa Uhuru na Mkuu wa Mkoa wa Pwani na Skauti Mkuu wa Chama cha Skauti Tanzania  Hajati Mwantum Mahiza (kushoto) katika uwanja wa ndege wa Terminal one (1) leo Jijini Dar es Salaam.
Picture 402 

Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam Said Meck Sadiki akitoa taarifa fupi mara baada ya kupokea Mwege wa Uhuru leo Jijini Dar es Salaam katika uwanja wa ndege wa Terminal one.
Picha na Hassan Silayo-MAELEZO

Despite welcome progress, childhood diseases remain major threat in sub-Saharan Africa

murray-chris-speaking-gbd-2010WASHINGTON, September 4, 2013Children in sub-Saharan Africa are now less likely to die from diarrhea and pneumonia, but these illnesses are still the most common causes of childhood death and sickness in most African countries, according to a new report published today.
Loss of health due to diarrheal diseases dropped 34% between 1990 and 2010, lower respiratory infections (LRIs) such as pneumonia dropped 22%, and protein-energy malnutrition was down 17%. Several countries documented striking progress, with Malawi reducing diarrheal diseases by 65%, Burundi decreasing LRIs by 44%, and Benin reducing measles by 84% during this time.

Malaria and HIV/AIDS were the leading causes of premature death and disability in 2010 for the region. But in some countries, there has been significant progress in recent years. Between 2000 and 2010, Rwanda recorded a 56% decrease in the rate of healthy years of life lost from malaria, while Botswana cut the rate of premature death and disability from HIV/AIDS by 66%.
These are some of the findings from the new report The Global Burden of Disease: Generating Evidence, Guiding Policy – Sub-Saharan Africa Regional Edition, published today by the World Bank and the Institute for Health Metrics and Evaluation (IHME).
“The rapid shifts in disease burden place poor people in low- and middle-income countries at high risk of not having access to appropriate services and incurring payments for health care that push them deeper into poverty,” said Timothy Evans, Director of Health, Nutrition, and Population at the World Bank Group. “The data in these new reports are critical inputs to the efforts of policymakers in countries towards universal health coverage that aim to improve the health of their people, communities, and economies.”
The report also finds that nutritional deficiencies were the leading cause for disability in childhood, mental and behavioral disorders accounted for the most illness during adolescence and young adulthood, while musculoskeletal disorders were the largest drivers of disability in adulthood.
In the region’s upper- and middle-income countries, non-communicable diseases emerged as a significant health threat. From 1990 to 2010, substantial increases in premature mortality and disability were recorded from stroke (up by 31%), depression (up by 61%), diabetes (up by 88%), and ischemic heart disease (or coronary artery disease, up by 37%). Amidst the region’s rapid economic growth, early death and illness from road injuries increased by 76% between 1990 and 2010. Health loss from interpersonal violence also climbed during this time, particularly in the Democratic Republic of the Congo and Lesotho.
The health landscape in sub-Saharan Africa is changing in unexpected ways,” said Dr. Christopher Murray, IHME Director and one of the lead authors of the GBD study. “Addressing chronic disease and certain communicable diseases will continue to be important, but people in sub-Saharan Africa are dealing with a greater range of illnesses today that aren’t fatal but are definitely disabling.”
The report also identifies trends in leading risk factors that cause the most disability in the region. Under-nutrition during childhood and household air pollution were among the leading factors behind premature death and disability.
Detailed findings for Sub-Saharan Africa and each country in the region are available online in a series of country profiles and data visualization tools.

NAOMBA RADHI KWA PICHA HII

 
NAWAOMBA RADHI KWA PICHA HII LENGO KUFIKISHA UJUMBE HII YA KUWACHOMA MOTO WEZI SI KATIKA MAFUNDISHO YA DINI YETU HAIFAI KWA UTUKUFU WA KIUMBE MWANAADAMU HUU NDIO UISLAM.

DAMU YA MUISLAMU ISIMWAGWE ISIPOKUWA KWA SABABU TATU

http://www.alneami.net/scriptalneami/40na/Images/14.gif

Kutoka kwa Ibn Mas'ud Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake amesema: Mtume
(S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani.
Damu ya Muislamu haiwezi kuwa haki kumwagwa isipokuwa katika hali tatu:  Mzinzi Muolewa (Mtu  mzima aliyeoa/olewa), uhai kwa uhai (nafsi kwa nafsi) na kwa     yule    anaewacha dini  na akajifarikisha na  jamaa (kundi) (amejitenga na watu wa dini yake).

HATOAMINI MMOJAWENU…


http://www.alneami.net/scriptalneami/40na/Images/13.gif
Kutoka kwa Abu Hamza Anas Ibn Malik    Radhi za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani     
mtumishi wa Mtume wa M/MUNGU Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani  alisema kwamba Mtume (S.A.W) Rehma za M/Mungu zimshukie Juu yake na Amani   kasema:
Haamini mmoja wenu (kikwelikweli) mpaka atakapompendelea ndugu yake kile anachojipendelea nafsi yake.
Hadithi hii Imesimuliwa na Al-Bukhari na Muslim

AJALI YA SHEIKH MUHAMMAD BAKARI DUMILA,MOROGORO M/MUNGU AMPE AFYA NJEMA DAIMA , NA AWAPOKEE MAPOKEZI MEMA MTOTO WAKE NA MKEWE ALIYE TANGULIA KATIKA AJALI HIYO NA WAISLAM WOTE KWA UJUMLA.

 
Sheikh Muhammad Bakar Al burhan, Mudir wa Madrasatil Shamsul maarif ya Tanga.
 
Zilikuwa ni Taarifa  za kushtua na Msiba Mkubwa kwa Waislam wa Tanzania na Afrika Mashariki Pale Mmoja katika Masheikh wetu Sheikh Muhammad Bakar Al burhan, Mudir wa Madrasatil Shamsul maarif ya Tanga,Alipopata ajali maeneo ya Dumila Mkoa wa Morogoro majira saa 8 mchana.

Ajali hiyo ilimsababishia majeraha  Sheikh Muhammad bakari katika maeneo ya kichwani,kifuani na mikononi.


Na vilevile wengine kupata Majeraha ambao walikuwa katika Msafara huo ambao walikuwemo Mwalimu Mussa Kunema,Idd issa Nori na kambi salum.


Msafara huo Sheikh aliongozana na watoto wake Abdulhalim,Ahmad, Abuubakar pamoja na mkewe. 


Msafara huo ulikuwa unatokea Tanga kwenda kondoa kwa ajili ya kutangaza dini.

Majeruhi wote walikimbizwa katika hospitali kuu ya Morogoro na baada ya hapo wali hamishwa kupelekwa hospital kuu ya Muhimbili.


Katika Ajali hiyo  Mtoto wa Sheikh aitwaye Abuubakar alifariki pamoja na mke mdogo wa sheikh bi ziyada naye amefariki.

Tunamwomba mwenyezi mungu amfanyie wepesi na kupona kwa haraka sheikh wetu na majeruhi wengine.


Vile vile  Mwenyezi mungu awapokee mapokezi mema na awasamehe makosa yao Marehemu zetu wote pia awaingize katika Pepo yake ya Darja ya Juu kabisa.

Amiin 
SHEIKH MUHAMMAD BAKAR ATOKA HOSPITALI.
 
Asubuhi ya Siku ya  Jumamosi Sheikh  ambae pia ni  mudir wa Madrasatul Shamsul maarif ya Tanga Sheikh Muhammad Bakar Al burhan alitolewa katika hospitali ya taifa ya Muhimbili.Sheikh alitolewa baada ya kupata nafuu kubwa pamoja na maendeleo mazuri ya afya yake.

Sheikh alikuwa amelazwa hospitalini hapo tangu siku ya jumanne ya Tarehe 27 akitokea katika hospitali ya mkoa wa morogoro kufuatia ajali ya gari aliyoipata wilaya ya dumila mkoani morogoro.

Aidha kwa sasa Sheikh ametakiwa na madaktari wa MOI waliokuwa wakimtibia kupata muda zaidi wa kupumzika ili kuimarisha zaidi afya yake.
Majeruhi wengine waliopewa ruhusa  ni Mwalimu Mussa kunema na Kambi Salumu.

Majeruhi Idd Issa Nori bado yupo hospitali ya Muhimbili wodi ya sewahaji akiendelea kupata matibabu zaidi.

Wakati huo huo imetolewa meseji ya mwisho ya marehemu Abubakar mtoto wa sheikh Muhammad Bakar,aliyoituma siku moja kabla hajafariki katika ajali hiyo ya Dumila.Meseji hiyo aliituma muda wa saa nane za mchana,sawa na muda aliofariki siku iliyofuata.

Baadhi ya watu aliowatumia meseji hiyo ni ustaadh Walid Alhad,imam wa msikiti wa kichangani pamoja na wanafunzi wenzake aliokuwa anasoma nao kwa Sheikh Alhad omar,Magomeni dar es salaam katika madrasatul Tadhwamun.

Meseji hiyo ambayo kama ilikuwa ikibashiri kifo chake na yenye ujumbe mzito wenye kuhitaji kuzingatiwa ilisomeka hivi;

"A,aleykum Pendelea saana kuhudhuria ktk mazishi na usisimame mbali na kaburi kuwa jirani nalo ili uione thamani yetu inavyokuwa baada ya kufa maana ile nguo tunayovishwa huwezi kuivaa ktk uhai na tunaviringishwa kwenye mkeka si tena kitanda kizuri ulichokuwa unalalia kisha tunaingizwa kwenye kishimo kirefu (MWANANDANI) na tunafukiwa udongo juu,hivi thamani yetu iko wapi? mpaka tunashindwa kumuabudu aliyetuumba tatizo nini,muda hatuna? au tatizo ujana?
Kama ujana, vijana wangapi wanaotangulia mbele ya haki kabla ya wazee? kama ni mzee unangoja nini wakati uzee ni dalili ya ukomo wa umri wako? Ni vema tukajiandaa mapema kwa sababu safari ni lazima insha allah mchana mwema".

Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis A. Mwamunyange Awavisha Nishani Maofisa wa Jeshi kwa Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Tanzania.

PICHA MBALI MBALI KATIKA SHEREHE ZA KUWATUNUKU NISHANI WANAJESHI ZANZIBAR.

Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis A. Mwamunyange, akiwasili katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai, akiwa na Mkuu wa Brigedi ya Nyuki Zanzibar, tayari kwa kuwavisha Nishani Maofisa ya Jeshi Tanzania kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu  wa Majeshi Tanzania Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania  Jakaya Mrisho Kikwete. sherehe hizo zimehudhuriwa na Familia za Maofisa hao na Wananchi.
Mkuu wa Majeshi Tanzania Davis A.Mwamunyange akipokea gwaride maalum liloandaliwa katika sherehe hizo za kutowa Nishani kwa Maofisa ya JWTZ katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.
Wapiganaji wa JWTZ wakipita mbele ya Mgeni Rasmini wa sherehe za kuwatunukia Nishani  Maofisa wa JWTZ , katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.

MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania LT COL M.K.Saburi. kwa niaba ya Amiri, Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Zanzibar
MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu Tanzania Meja II.Iddi, kwa niaba ya Amiri, Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Zanzibar
MKUU wa Majeshi Tanzania Davis Mwamunyange, akimvisha Nishani ya Utumishi Mrefu na Tabia Njema Tanzania Staf Sajeti Saida Mohammed,kwa niaba ya Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi Tanzania Rais Jakaya Mrisho Kikwete, sherehe hizo zimefanyika katika viwanja vya Kambi ya Jeshi Bavuai Migombani Zanzibar.
Wananchi na Wanafamilia wakihudhuria sherehe za kuvishwa Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Maosisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania.

Wageni waalikwa katika sherehe za kuwavisha Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Maofisa wa Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ) katika viwanja vya kambi ya Iddi Bavuai migombani Zanzibar.
Maafande wa JWTZ wakiwa na furaha baada ya kuvalishwa Nishani ya Utumishi Bora nawa Muda Mrefu Tanzania katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar.


Mkuu wa Majeshi Tanzania Devis A.Mwamunyange akiwa katika picha ya pamoja na Maofisa wa Jeshi la Wananchi waliotunikiwa Nishani ya Utumishi Bora na wa Muda Mrefu Tanzania, sherehe iliofanyika katika viwanja vya Kambi ya Iddi Bavuai Migombani Zanzibar. 

MKUU WA MAJESHI JENERALI MWAMUNYANGE AWATUNUKU NISHANI MAAFISA WA JESHI ZANZIBAR

Jenerali Davis Adolf Mwamunyange
Jenerali Davis Adolf Mwamunyange

Na Amina Abeid (ZJMMC)   3/9/2013.
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi ya Wananchi wa Tanzania (JWTZ) Jenerali Davis Adolf Mwamunyange leo amewatunuku Nishani Maafisa na Askari 39 wa JWTZ katika hafla iliyofanyika Kambi ya Jeshi ya Bavuai nje kidogo ya mji wa Zanzibar.
Mwamunyange amefanya zoezi hilo kwa niaba ya Rais wa Jamuhuri wa Muungano wa Tanzania na Amiri Jeshi Mkuu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na kufanya Idadi ya Wanajeshi waliotunikiwa Nishani msimu huu kutimia 939 Tanzania kwa ujumla.
Zoezi hilo limefanyika kwa Maafisa na Askari Jeshi wenye sifa za kulitumikia Jeshi kwa muda mrefu na kwa tabia ya kuweza kusifika katika Jeshi hilo.
Katika Zoezi hilo Maafisa wawili walitunikiwa Nishani ya Utumishi uliotukuka, Maafisa sita Wametunukiwa Nishani ya muda mrefu ambapo  Askari 31 wametunukiwa nishani ya tabia njema.
Akifafanua kuhusu Nishani hizo Mwamunyange amesema Nishani ya Utumishi uliotukuka hutolewa kwa Maafisa wenye cheo cha Meja kwenda juu ambao wametumikia Jeshi kwa miaka isiopungua 20 mfululizo.
Amesema Nishani ya Utumishi mrefu hutolewa kwa Maafisa na Askari wa JWTZ ambao wametimiza utumishi usiopungua miaka 15 mfululizo na nishani ya Utumishi mrefu na tabia njema huvishwa Askari wa JWTZ waliotumikia Jeshi mfululizo kwa muda usiopungua miaka 15.
Mkuu huyo wa Jeshi amesema Utaratibu huo wa kutunuku nishani umekuwa ukifanywa kwa muda mrefu kwa lengo la kupata Viongozi na Makamanda bora wa Jeshi ambao wametumikia Taifa lao kwa uaminifu na uzalendo wa hali ya juu.
Kwa upande wake mmoja wa Watunukiwa wa Nishani ya Utumishi wa Muda mrefu na tabia njema Saida Said amesema, amefarajika kupata nishani hiyo kwani itamtambulisha Jeshini kuwa ana tabia njema.
Zoezi la kutunuku nishani kwa Maafisa na Askari wa JWTZ limefanyika katika kituo cha KJ 12,Zanzibar na linatarajiwa kuendelea kwa vituo vingine nchi Nzima.

Balozi Seif akutana na Waziri wa habari wa Oman

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akizungumza na Ujumbe wa Serikali ya Oman ukiongozwa na Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani hapo Ofisi kwake Vuga Mjini Zanzibar.
Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani akiagana  na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi mara baada ya ujumbe wake kuzungumza nae hapo Ofisini kwake  Mtaa wa Vuga Mjini Zanzibar.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiwa pamoja na Ujumbe wa Serikali ya Oman ambao pia upo Zanzibar kushiriki Kongamano la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiislamu.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Habari wa Nchi Hiyo Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani  na kushoto yake ni Waziri wa Habari, Utamaduni, Utalii na Michezo Zanzibar  Said Ali Mbarouk.
Picha na Hassan Issa wa – OMPR – ZNZ.


Na Othman Khamis Ame, OMPR
 
Uhusiano wa  kubadilishana nyaraka za Kihistoria kati  ya Oman na Zanzibar  unaweza kuwasaidia wananchi  wa pande  mbili  pamoja na watafiti wa masuala ya Kihistoria kuelewa kwa kina maingiliano ya muda mrefu yaliyopo kati ya  Wazanzibar na Waoman ambayo yanafanana  Kisilka na Kiutamaduni.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema hayo wakati wa mazungumzo yake na Ujumbe wa Viongozi sita wa Serikali ya Oman ulioongozwa na Waziri wa Habari wa Nchi hiyo Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani aliokutana nao hapo Ofisini kwake Vuga Mjini Zanzibar.
 
Balozi Seif alisema Zanzibar na Oman zimekuwa na uhusiano wa Kihistoria wa muda mrefu tokea karne ya 18 ambao umethibitishwa na wataalamu pamoja na watafiti wa mambo ya Kihistoria kutoka vyuo vikuu tofauti Duniani.
 
Alielezea haja kwa Viongozi na Wananchi wa Oman na Zanzibar kuendelea kushikamana na kushirikiana katika masuala mbali mbali ya maendeleo yatakayosaidia ustawi wa vizazi vya sehemu zote mbili rafiki.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar aliipongeza Serikali ya Oman  kupitia ushirikiano wa mamlaka  ya kumbu kumbu na nyaraka ya Oman na Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar { SUZA } kwa kuandaa Kongamano la Kimataifa la Ustaarabu wa Kiiislamu kwa Nchi za Mashariki mwa Bara la Afrika.
 
Balozi Seif alisema  uamuzi huo wa kufanywa kwa kongamano hilo  hapa Zanzibar umekuja wakati muwafaka kwa wataalamu wa mambo ya Kale kubainisha kwamba  Historia ya Uislamu imeanzia hapa Zanzibar.
 
“ Nimefurahi kusikia kwamba Historia ya Uislamu imeanza Zanzibar. Inaonyesha watafiti wameliona hili kutokana na asilimia kubwa ya wakaazi wa Visiwa vya zanzibar  kuwa  waumini wa Dini ya Kiislamu sambamba na Utamaduni wake “. Alieleza Balozi Seif.
 
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alishauri tafiti za Wataalamu wa masuala ya Historia ambazo zitaibuka katika Kongamano hilo  zielekezwe zaidi kunufaisha wananchi  na waislamu wa ukanda wote wa Afrika Mashariki.
“ Tafiti hizi za Wataalamu wetu wa Kihistoria itapendeza kama zitaendelea kubakishwa katika maktaba zetu ili zisaidie wananchi, waislamu na hata wasomi wetu wa vyuo vikuu vya ukanda wetu wa Afrika Mashariki “. Alisisitiza Balozi Seif Ali Iddi.
Naye Kiongozi wa Ujumbe huo wa Serikali ya Oman Waziri wa Habari wa Nchi hiyo   Dr. Abdulmumin Mansour Bin Said Al- Hasani alisema ipo haja ya kuendelea kuhifadhiwa kwa Historia iliyopo ya Zanzibar na Oman kwa faida ya vizazi vijavyo.
 
Dr. Abdulmumin alieleza kwamba upeo wa tabia za watu wa oman na Zanzibar unaolingana ndio unaochangia na kushawishi wageni na watalii wa mataifa mbali mbali  duniani  kupendelea kuzitembelea nchi hizi zinazofanana kiutamaduni.
 
Waziri huyo wa Habari wa Oman alifahamisha kwamba Kongamano  hilo la ustarabu wa Kiislamu linalofanyika hapa Zanzibar  mbali ya utafiti uliopatikana lakini pia litafungua uhusiano katika Nyanja nyengine za maendeleo kwa nchi shiriki.
 
Dr. Abdulmumin alielezea faraja yake kutokana na umuhimu wa udugu uliopo  kati ya watu wa Oman na Zanzibar ambao umepelekea waoman wengi  kujitokeza kushiriki kwenye kongamano hilo.
 
Alifahamisha kwamba ipo ishara ya kuendelea kwa ziara za mara kwa mara kati ya watu wa pande hizo mbili.
 
Kongamano hilo la siku tatu linalofanyika katika Hoteli ya Kimataifa ya La Gemma Della East Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na kushirikisha Mataifa yapatayo 17 lina lengo la kuitangaza Zanzibar katika Nyanja za utafiti na Taaluma Kimataifa.
 
Hilo ni kongamano la Pili la Kimataifa la Ustarabu wa Kiislamu  kufanyika likitanguliuwa na lile la mwaka 2012 lililofanyika Nchini Uganda na kutolewa uamuzi wa kongomano linalofuata kufanyika hapa Zanzibar kutokana na  Historia yake  iliyopo  sambamba na uhusiano  wa karibu iliyonayo na Mataifa ya Kiarabu.

TASWIRA KUTOKA KITUO CHA MABASI MAKUMBUSHO

Muonekano wa kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini Dar.

Kamera zetu leo zimeelekea katika kituo cha mabasi cha Makumbusho jijini Dar, ambapo licha ya kuwa na eneo kubwa na mazingira safi kama kituo cha daladala kinavyostahili, ni daladala na abiria wachache ndiyo wameonekana kufika katika kituo hicho tofauti na vituo vingine vilivyopo katika barabara ya New Bagamoyo.
Picha na Habari kwa Hisani ya  Chande Abdallah / GPL

MABILIONEA 10 WANAOTIKISA TANZANIA

MABILIONEA 10

KATI ya miaka ya 1960 hadi 1980, mtu kuwa tajiri alionekana ni hatari kwa taifa, tena mali zake alizimiliki kwa kificho, vinginevyo angeitwa mhujumu uchumi. Lakini kwa sasa mambo yamebadilika, taratibu sera za kibepari zinatawala, ujamaa unapewa kisogo.
Dk. Reginald Mengi.
Mtu kama ni mbunifu, ana nidhamu ya kutofuja pesa na anafanya kazi sana kwa nini asiwe tajiri? Utandawazi unasaidia ndiyo maana leo tunaweza kuwatambua mabilionea wakubwa ambao wanastahili pongezi kwa hatua walizopiga. Tusisahau kuwa wanaibeba nchi kwa ulipaji kodi.
 

 Said Salim Awadh Bakhresa.
1. SAID BAKHRESA
Jina lake kamili ni Said Salim Awadh Bakhresa. Jarida la Forbes mwaka jana, lilimuorodhesha miongoni mwa matajiri 40 Afrika kwamba anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 620 (karibu shilingi trilioni moja). Hata hivyo, inadaiwa kuwa tabia ya usiri wa Bakhresa inafanya mali zake zisijulikane sana, ila ni tajiri zaidi ya kiwango hicho.
Ndiye mmiliki wa makampuni ya Bakhresa yanayotoa bidhaa zenye chapa ya Azam ambazo zinauzwa nchi mbalimbali Afrika. Ana viwanda vya nafaka na vinywaji, vyombo vya usafiri wa majini, uuzaji wa chakula, bidhaa za plastiki na kadhalika. Ndiye mmiliki wa Klabu ya Azam FC.


2. GULAM DEWJI
Huyu ni baba wa mfanyabiashara maarufu nchini, Mohamed Dewji ‘Mo’. Jarida la Forbes mwaka jana lilimtaja kuwa na utajiri wenye thamani ya dola milioni 560 (karibu shilingi bilioni 900). Mafanikio yake kibiashara yalianza mwaka 1970. Kiwanda chake cha 21st Century Textiles, kinatajwa kuwa moja ya viwanda vikubwa vya nguo Afrika.
3. ROSTAM AZIZ
Inadaiwa anamiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 420 (shilingi bilioni 672). Anamiliki karibu asilimia 40 ya hisa Kampuni ya Vodacom Tanzania. Ni mmiliki wa Kampuni ya Caspian inayohusika na uchimbaji wa madini na ukandarasi nchini Tanzania, nchi kadhaa za Afrika na Asia.
4. DK. REGINALD MENGI
Anatajwa kumiliki utajiri wenye thamani ya dola milioni 280 (karibu shilingi bilioni 450). Ni mmiliki wa kundi la makampuni ya IPP, yanayomiliki vyombo vya habari, viwanda, migodi ya dhahabu, Tanzanite na kadhalika.
5. ALI MUFURUKI
Utajiri wake unatajwa kuwa na thamani ya dola milioni 110 (shilingi bilioni 176). Ni mmiliki wa kundi la makumpuni ya Infortech Investment, inayomiliki maduka yanayouza vitu vya rejareja Tanzania na Uganda. Vilevile ana vitega uchumi vingine.
6. MUSTAFA SABODO
Ni mfayabiashara mkubwa sana nchini anayemwaga mamilioni kwa misaada. Wakati wa kuanzishwa kwake, aliipa Taasisi ya Mwalimu Nyerere shilingi milioni 800, akasaidia shilingi milioni 100 katika mradi wa kustawisha mimea jamii ya kunde. Vilevile alikipa Chadema shilingi milioni 300. Inadaiwa kuwa utajiri wake unazidi shilingi bilioni 100. Kampuni yake ya Khoja Shia Itnasheri Jamat (KSIJ), ndiyo yeye tenda ya kujenga maeneo ya maegesho ya magari Posta, Dar es Salaam, mradi wenye thamani ya shilingi bilioni 5.6.
7. ABDUL-AZIZ ABOOD
Kiwango chake cha utajiri hakiwekwi sana wazi lakini anatajwa kuwa miongoni mwa mabilionea 10 wanaotikisa nchi kwa sasa. Anamiliki viwanda kadhaa mkoani Morogoro, vyombo vya habari, Abood Radio na TV. Anamiliki mabasi ambayo yanafanya safari zake kati ya Morogoro, Mbeya na Dar es Salaam. Ni Mbunge wa Morogoro Mjini (CCM).
8. MICHAEL SHIRIMA
Ni mmiliki mkuu wa Shirika la Ndege la Precision ambalo linafaya safari zake ndani ya Tanzania pamoja na nchi mbalimbali za Afrika. Ana asilimia tano ya hisa katika Beki ya I&M (Tanzania), vilevile ni memba katika bodi ya wakurugenzi wa benki hiyo yenye thamani ta shilingi bilioni 200. Hisa zake Precision ni asilimia 42.91.
9.  YUSUF MANJI
Kiwango halisi cha utajiri wake bado hakifahamiki lakini anafahamika kama mmoja wa mabilionea wakubwa nchini Tanzania. Ni mmiliki wa makampuni ya Quality Group na majengo ya Quality Centre, Quality Plaza na kadhalika. Ni Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga na utajiri wake umeifaya timu kutotetereka tangu alipoanza kuiongoza.
10. MOHAMMED DEWJI
Baba yake anashika nafasi ya pili katika orodha hii. Dewji au Mo kama anavyoitwa na wengi, anatajwa kuwa bilionea nambari moja katika orodha ya mabilionea vijana Afrika (orodha hiyo tuliitoa wiki iliyopita). Ni mmiliki wa makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (METL) ambayo inatengeneza faida ya shilingi bilioni 136 kwa mwaka.

JWTZ YAPELEKA KILIO RWANDA

*Yakamata maofisa wake wanne wa Kijeshi
*M-23 wakiri majeshi ya UN ni hatari yatawamaliza

ASKARI wa Umoja wa Mataifa wanaolinda amani nchini Kongo (Monusco), wakiongozwa na vikosi vya Jeshi la Wananchi Tanzania (JWTZ), wamedai kuwakamata maofisa wanne wa jeshi la Rwanda, katika mapigano ya wiki iliyopita nchini Kongo.

Akizungumza na MTANZANIA Jumatano kwa sharti la kutotajwa jina, mmoja wa askari aliyepo ndani ya kikosi cha JWTZ huko nchini Kongo, alisema maofisa hao wanashikiliwa kwa mahojiano zaidi.

Taarifa hizi za sasa zinakuja wakati ambapo kumekuwa na madai ya muda mrefu, ambayo yamekuwa yakitolewa na Umoja wa Mataifa pamoja na Marekani kwamba, Rwanda imekuwa ikiwasaidia waasi wa kundi la M-23.

Pamoja na kwamba Rwanda imekuwa ikipinga madai hayo, kitendo chake cha wiki iliyopita cha kuamua kupeleka bataliani mbili zenye wanajeshi 1,700 ili kukabiliana na kile kinachodaiwa kuwa ni kishindo cha vikosi vya Umoja wa Mataifa vyenye jukumu la kulinda amani katika taifa hilo lenye utajiri mkubwa kirasilimali, kinatokana na waasi wa M23 kupata kipigo kikali.

Chanzo chetu hicho kutoka uwanja wa mapambano nchini Kongo, kililidokeza gazeti hili kuwa maofisa hao wa Jeshi la Rwanda waliwakamata katika mapigano hayo yaliyodumu kwa zaidi ya wiki moja, ambayo tayari yamewakimbiza waasi wa M23.

“Askari wa Rwanda tuliowakamata, ni maofisa wa ngazi za juu kabisa jeshini, tena walikuwa na sare za jeshi hilo… walikuwa wakiwasaidia hao M23, lakini kwa kuwa sisi tulikuwa makini tulifanikiwa kuwatandika hadi tukawakamata,” kilisema chanzo chetu hicho.

Habari za uhakika kutoka vyanzo vya habari vya kuaminika zinaeleza kwamba, hatua hiyo ya kuwakamata maofisa hao pamoja na kuondoka kwa waasi wa kikundi cha M23, imefanikisha kushinda vita hiyo kwa zaidi ya asilimia 95.

Mtoa taarifa wetu huyo kutoka Kongo, ameliambia gazeti hili kuwa, tayari Monusco wanaoongozwa na JWTZ wameanza kufurahia ushindi huo na kwamba sasa hivi wanasubiri tamko kutoka kwa wakuu wao, ili kufahamu kinachofuata baada ya kufanikisha hatua hiyo.

MAPIGANO YALIVYOKUWA
Akielezea namna walivyofanikiwa kutoa kibano kwa M23, askari huyo kwanza alikiri kuwa mapigano yalikuwa makali, kutokana na kikundi hicho cha waasi kusheheni vifaa vya kisasa na msaada wanaoupata kutoka Serikali ya Rwanda.

“Kwa kweli mapigano yalikuwa makali sana, lakini kwa upande wetu sisi tulikuwa tunajiamini kutokana na vifaa ambavyo pia ni vya kisasa hususani ikizingatiwa jeshi letu ni la Umoja wa Mataifa.

“Tulifanikiwa kuteka ngome yao kwa kutumia mbinu mbalimbali za kijeshi na kuwafanya watawanyike kabisa katika eneo hilo.

“Ngome yao ilikuwa ni kubwa sana, ina ukubwa wa zaidi ya viwanja vitatu vya mpira… na katika eneo hilo kulikuwa kumesheheni vifaa vyao vya kivita, kama makombora, mafuta, mizinga pamoja na vifaa vingine kama magari na baadhi ya silaha nyingine kubwa kubwa za kivita,” alisema.

Alisema kutokana na hali hiyo, sasa hali ni shwari ndani ya nchi hiyo ya Kongo.

“Baada ya kuwasambaratisha sasa wamekimbilia eneo moja lililopo karibu na mpaka wa Uganda. Kama unavyofahamu hawa jamaa walikuwa wakitumia mbinu za kujihami kwa kurusha mabomu katika eneo la Rwanda, ili ionekane kuwa sisi tumerusha,” alisema askari huyo.

“Lakini tunamshukuru Mungu, tupo salama ingawa tumempoteza askari mmoja na askari wengine wenzetu wa Tanzania ambao ni wanne, wamepata majeraha kidogo lakini wanaendelea vizuri.

“Hivyo nawaomba Watanzania wenzangu waendelee kutuombea turudi salama, kwa sababu kazi sasa imeshakamilika,” alisema askari huyo.

Juhudi za gazeti hili kumpata msemaji wa Monusco, Luteni Kanali Prosper Basse kuzungumzia juu ya taarifa hizo, zilishindikana.

Taarifa ambazo tumezinasa kwa siku kadhaa sasa kutoka uwanja wa mapambano na ambazo zimegusa vichwa kadhaa vya habari zinaeleza kuwa, brigedia maalumu ya vikosi vya UN yenye dhamana ya kujibu mashambulizi (FIB), katikati ya wiki iliyopita iliendesha operesheni kubwa iliyoharibu kabisa ngome muhimu ya waasi wa M23, hali inayotajwa na wachambuzi wa mambo kuwa ndiyo iliyoishtua Serikali ya Rwanda ambayo inatuhumiwa kuwasaidia waasi hao.

Taarifa za kijeshi zinaeleza kuwa, FIB ambayo inaundwa na wanajeshi wapatao 3,000 kutoka Tanzania na Afrika Kusini chini ya Azimio Namba 2098 la Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, limejizatiti kwa zana za kisasa za kivita zikiwamo mizinga na helikopta za kivita.

Taarifa kutoka mashariki ya Kongo zinaeleza kwamba, mashambulizi dhidi ya waasi wa M23 ambao hivi karibuni waliripotiwa kusababisha kifo cha mwanajeshi mmoja wa Tanzania aliye katika jeshi la UN, yamesababisha waasi hao kukimbilia katika eneo la milima lililopo umbali wa kilomita tano kutoka mji mdogo wa Kanyaruchinya Mashariki mwa Goma.

M23 WAZUNGUMZA
MTANZANIA Jumatano jana lilifanikiwa kuzungumza na Rais wa M23, Bertrand Bisiimwa, ambapo pamoja na mambo mengine alieleza sababu za vikosi vyao kuondoka katika ngome yao ya kivita sambamba na taarifa za kuibuka kwa mapigano mapya ya hivi karibuni.

Katika hilo, Bisiimwa alikiri kikosi chake kurudi nyuma siku nne zilizopita, huku akiitaja sababu ya kufanya hivyo kuwa ilitokana na wao kutotaka vita baada ya majeshi ya Kongo kuanza kuwarushia mabomu kwenye kambi yao.

“Sisi tuliamua kurudi nyuma tusiendeshe vita, tunajua aliyetupa hayo mabomu ambayo yalifika mpaka Rwanda, tunaitaka Umoja ya Mataifa ikuje ifanye uchunguzi wake…wakuje waangalie vifaa yetu waone kama inaweza kurusha mabomu hadi Rwanda,” alisema.

Hata hivyo, Bisiimwa alisema kuwa sio kweli kama majeshi ya Umoja wa Mataifa yakiongozwa na JWTZ yaliwasambaratisha katika ngome yao.

“Sio kweli walikuja Kanyaruchina tukiwa tumeondoka na tuliondoka si kwa sababu ya kuwakimbia, hapana tulitaka UN wafanye uchunguzi yake juu ya kurushwa mabomu, kwa sababu wanataka kutuvalisha mambo ya uongo mchafu,” alisema Bisiimwa.

Bisiimwa alijigamba kuwa majeshi ya Kongo hayawawezi na kwamba walikwishawashindwa, lakini akakiri kwamba majeshi ya Umoja wa Mataifa wanaweza kuwaondoa.

“Ninakiri hiyo kwa sababu Umoja wa Mataifa inaweza kututoa, unajua inakuwa na nguvu ya hatari,” alisema Bisiimwa kwa Kiswahili cha tabu.